Kiungo wa Yanga sc Khalid Aucho maarufu kama Daktari wa mpira atakosa michezo yote miwili ya fainali ya kombe la shirikisho barani Africa baada ya kupata kadi 6 za njano kwenye mashindano hayo tangu msimu huu uanze kwa ujumla wake.
Kwenye michuano hii ya Caf kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo ya pili kwa ukubwa barani Afrika kwa ngazi za klabu ukipata kadi mbili za njano unakosa mchezo mmoja,lakini ukipata jumla ya kadi 6 za nanjo unakosa michezo miwili ivyo Aucho yeye amepata idadi ya jumla ya kadi 6 za njano huku kadi ya 6 aliipata kwenye mchezo wa dhidi ya Marumo Gallants kule Africa ya Kusini.
Yanga sc itakuwa na pengo kubwa kumkosa Aucho kwani amekua mhimili mkubwa katika eneo la kiungo la klabu hiyo ambapo amekua akitumika kama injini ya timu inapokua inashambulia na kuzuia huku uhakika wake wa pasi ukiwa ni mwiba kwa wapinzani wanaokutana nae uwanjani.
Hata hivyo kocha Nasredine Nabi bado anayo machaguo mengine katika eneo hilo ambapo yupo Stephane Aziz Ki,Mudathiri Yahya,Farid Musa na Salum Abubakar huku pia anaweza kumtumia Yannick Bangala katika eneo hilo.
Yanga sc itavaana na Usm Algers katika mchezo wa fainali ya kombe la shirikisho wakianzi hapa nchini siku ya Jumapili Mei 28 na marudiano itakua Juni 3 nchini Algeria.