Home Makala Simba sc Yaangusha Alama Kagera

Simba sc Yaangusha Alama Kagera

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba sc imeshindwa kupata ushindi katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera sugar baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 katika mchezo wa raundi ya 17 uliofanyika katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Kagera Sugar walikua wa kwanza kupata bao la mapema dakika ya 15 ya mchezo likifungwa na Dennis Bukenya aliyemlizia mpira wa kona ambao mabeki wa Simba sc walizubaa kuukoa ukielekea langoni taratibu lakini bao hilo lilidumu mpaka dakika ya 38 ambapo Henock Inonga alisawazisha kwa kichwa akiunganisha kona ya Cletous Chama.

Dakika 90 za mchezo huo zilimalizika kukiwa hakuna timu iliyofanikiwa kuongeza bao na kusababisha timu hizo kugawana alama moja moja na kuwafanya Simba sc kufikisha alama 37 wakiwa na michezo 17 ya ligi kuu katika nafasi ya tatu huku Kagera sugar wakiwa katika nafasi ya sita wakiwa na alama 27 wakicheza michezo 17 ya ligi kuu nchini.

banner

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.