Connect with us

Makala

Ntibanzokiza Atua Geita Sc

Aliyekua mchezaji wa klabu ya Yanga sc Saido Ntibanzokiza amekiunga na klabu ya Geita Gold SC inayoshiriki michuano ya ligi kuu nchini huku ikiwa na tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la shirikisho ambapo amejiunga kwa mkataba wa miaka miwili.

Saido aliyeshindwana na Yanga sc baada ya kumaliza mkataba wake huku kisa cha utovu wa nidhamu kambini jijini Mwanza wakati wa kuelekea mchezo wa nusu fainali dhidi ya Simba sc ikitajwa ndio chanzo cha kutopewa mkataba mpya licha ya kuwa na sababu zingine nyuma ya pazia.

katibu wa Geita Gold Simon Shija amethibitisha kufanikiwa kunasa saini ya Saido Ntibazonkiza “Katika kuboresha kikosi kuelekea mashindano ya kimataifa mwalimu alikua anahitaji mchezaji mwenye uzoefu ambae anaweza akakaa kwenye vyumba na akawaambia wachezaji na kuwapa experience ya mashindano ya kimataifa”

Moja ya jina alilopendekeza mwalimu ni Saido Ntibazonkiza na tumefanikiwa kumtimizia kile alichokihitaji. Kama mnavyofahamu Geita Gold ina wachezaji wengi vijana ambao watahitaji sana mchango wa mawazo kutoka kwa Saido Ntibazonkiza. Ninachotaka niueleze umma ni mpaka sasa Saido ameshakua mchimba dhabibu wa Geita.Alisema Simon Shija

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Makala