Monday, May 12, 2025
Home Makala Staika wa Simba sc Kucheza Siku ya Wananchi

Staika wa Simba sc Kucheza Siku ya Wananchi

by Sports Leo
0 comments

Makamu wa Rais  wa Yanga SC, Arafat Haji, ameeleza kuwa siku ya kilele cha wiki ya mwananchi Agosti 6 klabu hiyo itacheza mechi dhidi ya Vipers Fc kutoka Uganda.

Arafat, ameeleza hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar Es Salaam ambapo alithibitisha timu hiyo kuja nchini kushiriki mechi hiyo ambapo mshambuliaji Cesar Lobi Manzoki ni miongoni mwa mastaa watakaoshiriki mchezo huo licha ya varangati la usajili wake kujiunga Simba sc likiwa halijafika mwisho.

“Bingwa huwa anacheza na bingwa mwenzake kwahiyo kuelekea tamasha hili ambalo kilele chake kitakuwa ni Tarehe 6, timu yetu Young African Sports Club, tutacheza na mabingwa wenzetu wa kutoka Uganda, timu ya Vipers FC.

banner

“Nadhani wote mnaelewa Vipers ni mabingwa wa Uganda, na bingwa hadhi yake ni kucheza na bingwa mwenzake”Alisema Arafat ambaye ni makamu Rais wa klabu hiyo iliyobeba vikombe vyote msimu ulioisha.

Hiyo itakua ni nafasi ya wananchi na mashabiki wa soka nchini kupata nafasi ya kumuona staa huyo ambaye amekua maarufu kutokana na kuwaniwa na klabu ya Simba sc huku timu yake ya Vipers ikigoma kumuuza.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.