Connect with us

Makala

Mastaa Yanga sc,Azam Fc Ni Next Level

Ligi kuu nchini imezidi kupanda hadhi baada ya kuwa na mastaa wa uhakika ambao wanasifika katika nchi zao kuwa na viwango bora kiasi cha kupata tuzo za maana katika ligi kuu msimu uliopita.

Mastaa Stephane Azizi Ki na Tape Edinho ni miongoni mwa mastaa hao ambao wametwaa tuzo katika ligi kuu nchini Ivory Coast kutokana na kufanya vizuri  msimu uliopita kabla ya kuhamia kwa mabingwa hao wa nchini pamoja na walambalamba wa Azam Fc.

Katika tuzo za ligi kuu msimu uliopita kiungo Stephane Aziz Ki amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu nchini Ivory Coast baada ya kucheza kwa kiwango kikubwa katika klabu yake hiyo ya msimu uliopita ya Asec Mimosa ambapo alionyesha kiwango safi akifunga mabao matano katika michuano ya kimataifa.

Tape Edinho kiungo mshambuliaji aliyesajiliwa na Azam Fc akitokea nchini Ivory Coast nae ametwaa tuzo ya kuwa Mchezaji Bora anayetarajiwa kufanya makubwa (Meilleur Espoir De La Ligue 1) kwenye Ligi Kuu ya Ivory Coast (Ligue 1) msimu ulioisha.

Mastaa hawa wote wawili wanatarajiwa kufanya makubwa katika ligi kuu nchini kutokana na sajili hizo na viwango vyao wakati wakiwa katika nchi zao.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Makala