Kufuatia kufumuliwa kwa benchi la ufundi la klabu ya Yanga sc klabu hiyo ipo mbioni kumnsa kocha Mfaume Athuman ambaye kwa sasa ni kocha wa makipa wa timu ya Dodoma Jiji Fc.
Mfaume ambaye aliwahi kuidakia klabu ya Yanga sc hapo zamani anawindwa na Yanga sc ili kuchukua nafasi ya Vladmil Niyonkuru ambaye ametimuliwa pamoja na kocha Cedrick Kaze.
Mfaume tayari ameshakubaliana na Yanga sc mambo yote ya msingi lakini changamoto kubwa ni mkataba wake na klabu hiyo yenye maskani yake jijini Dodoma yalipo makao makuu ya nchi hivyo amepewa muda maalumu ili kumalizana na klabu yake hiyo.