Thursday, May 8, 2025
Home Soka Yanga sc Yazinduka Dodoma

Yanga sc Yazinduka Dodoma

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kuibuka na alama tatu muhimu katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma baada ya kuifunga timu hiyo kwa mabao 2-0.

Ikiingia uwanjani bila mastaa wake Khalid Aucho na Yannick Bangala ikiwaanzisha Djigui Diarra,Kibwana Shomari,Dickson Job na Bakari Mwamnyeto katika eneo la ulinzi huku Kiungo akiwa ni Zawadi Mauya,Salum Abubakari,Feisal Salum,Dickson Ambundo na Jesus Moloko huku Mshambuliaji akiwa ni Fiston Mayele ambapo dakika ya 14 Dickson Ambundo alifanikiwa kufunga bao la uongozi kwa shuti kali akipokea pasi ya Jesus Moloko.

Uzembe wa Kipa Mohamed Yussufu uliwazawadia Yanga sc goli la pili kutokana na uzembe wa kushindwa kuokoa shuti lililopigwa na Zawadi Mauya dakika ya 35 ambapo kipindi cha kwanza mchezo ulimalizika kwa sare na mpaka kipindi cha pili kinamalizika matokeo yalisalia hivyo licha ya kosa kosa za hapa na pale kwa pande zote huku Kipa Djigui Diarra akilazimika kufanya kazi ya ziada kuiweka Yanga sc mchezoni.

banner

Yanga sc imezidi kujichimbia kileleni ikiwa na alama 60 ikiwaacha Simba sc katika nafasi ya pili kwa alama 11 zaidi huku ikiwa na mchezo 24 ikisaliwa na michezo 6 ambapo itawavaa Mbeya kwanza jumapili ijayo.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.