Tuesday, May 13, 2025
Home Makala Simba sc Yatambulisha Jezi za AFL

Simba sc Yatambulisha Jezi za AFL

by Sports Leo
0 comments

Simba Sc imetambulisha jezi maalum zitakazotumika katika michuano ya African Football League (AFL) ikianza mechi ya ufunguzi ya robo fainali dhidi ya Al Ahly Oktoba 20 katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam.

Jezi hizo zimetambulisha mbele ya waandishi wa habari zikiwa katika rangi za kila siku za klabu hiyo nyekundu na nyeupe ambazo ndio rangi za asili za klabu hiyo.

Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na mwenyekiti wa klabu hiyo Murtaza Mangungu ambaye alielezea yafuatayo “Tupo imara, kila Mwanasimba atekeleze majukumu ili tufikie malengo yetu na kufikia hatua nzuri. Sandaland amekuwa mfano mzuri wa kazi anayofanya, mdhamini mkuu M-Bet, makampuni ya Mo na wadhamini wengine wote.”.

banner

Naye mwenyekiti wa bodi ya klabu hiyo Salum Abdalah Muhene alisema yafuatayo mbele ya waandishi wa habari “Nafurahi kuwambia baada ya uzinduzi wa jezi hii, jezi zitaanza kupatikana kwenye maduka ya Sandaland. Leo wataanza kupendeza. Nawaomba Wanasimba wanunue na wavae hata wageni wakifika wajue nchi hii ni Simba.”

“Tupo African Football League, tumewaacha wengine mbali. Muda ukifika pumba na mchele hujitenga.”Alisema Muhene ambaye pia anajulikana kwa jina maarufu la Try again.

Simba sc inatarajiwa kucheza na Al Ahly Fc katika ufunguzi wa michuano mipya ya African Football League itakayofanyika hapa nchini siku ya Oktoba 20 mwaka huu.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.