Connect with us

Makala

Baleke Mtu na Nusu

Akianza katika kikosi cha Simba sc kwa mara ya kwanza staa Jean Baleke aliifungia Simba sc bao pekee katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji Fc uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini humo.

Simba sc ikianza mchezo huo bila mastaa wake wa kikosi cha kwanza cha kila siku takribani tisa wakiwemo Cletous Chama,Mzamiru Yassin,Sadio Kanoute,Pape Sakho,Henock Inonga na Joash Onyango huku ikiwaanzisha Jean Baleke na Ismael Sawadogo katika kikosi hicho.

Licha ya kutoonesha kiwango kizuri kama ilivyo kawaida kikosi hicho kilifanya mashambulizi mara kwa mara langoni mwa Dodoma Jiji huku uzembe wa kipa wa timu hiyo ukimzawadia goli la pekee la mchezo huo Baleke dakika ya mwisho ya kipindi cha kwanza.

Dodoma jiji pamoja na kuahidiwa kiasi cha shilingi milioni moja na nusu kwa kila mchezaji kama wangepata ushindi katika mchezo huo lakini kutokana na uimara wa mabeki wa Simba sc mpaka dakika tisini ziliisha wakiwa wamepoteza mchezo huo.

Simba sc sasa imeiongezea presha Yanga sc ambapo imefikisha alama 50 nyuma ya Yanga sc yenye alama 53 kilele mwa ligi kuu huku Yanga sc wakiwa na mchezo mmoja mkononi ambao watacheza na Ruvu Shooting.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala