Connect with us

Soka

Ronaldo avunja rekodi ya mabao duniani

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Manchester United Cristiano Ronaldo amevunja rekodi ya mabao kwa timu za timu kwa soka la wanaume iliyokuwa inashikiriwa na Muiran Ali Ade.

Ali alikuwa akishikiria rekodi hiyo kwa muda mrefu ya kufunga mabao 110,kabla ya rekodi hiyo kuvunjwa na Ronaldo na kuweka nyingine mpya usiku wa kuamkia leo kwenye mechi ya kufuzu kombe la dunia dhidi ya Ireland.

Ronaldo alifunga bao la kuvunja rekodi dakika ya 89 na kufikia 110 yaliyofungwa na Ali kabla ya kufunga tena dakika ya 96 ya mchezo na kuweka rekodi mpya ya dunia ya mabao 111 na kuisaidia Ureno kuibuka na ushindi katika mchezo huo.

Mpinzani mkubwa wa Ronaldo Lionel Messi yupo nafasi ya tatu katika orodha hiyo akiwa na mabao 76 ngazi ya timu ya taifa.

Uwezo wa mshambuliaji huyo kuendelea kupachika mabao unazidi kuwapa jeuri mashabiki wa Manchester United ambao wanaamini kuwa ataenda kuisaidia idara ya ushambuliaji ya timu hiyo inayomtegemea zaidi Bruno Fenarndez.

Kabla ya mchezo huo kuanza Ronaldo alikabidhiwa tuzo ya mfungaji bora wa michuano ya Euro 2020 kwa kufunga magoli 5.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka