Kikosi cha Namungo kinaendelea na mazoezi makali kujiandaa na mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Nkana kutokea Zambia, huku wakitamba kuwa Wazambia hao lazima wadondoshe pointi tatu kwa Mkapa.
Ofisa Habari wa Namungo, Kindamba Namlia amesema: “Kikosi chetu kinaendelea vizuri na mazoezi ya kujiandaa na mchezo wetu wa Ijumaa dhidi ya wageni wetu Nkana kutokea Zambia.
“Mpaka sasa tumekamilisha asilimia kubwa ya maandalizi ya mchezo huo na tunasubiri muda wa mchezo ufike, kikosi chetu kiko kamili kwani idadi kubwa ya majeruhi tayari wamepona na wanaendelea na mazoezi japo tutaendelea kukosa huduma ya mshambuliaji wetu Bigirimana Blaise ambaye amekuwa na majeraha ya muda mrefu.”
.