Connect with us

Makala

Ngorongoro Heroes Yatwaa Ubingwa Cecafa

Timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 20 imefanikiwa kutwaa ubingwa wa kombe la vijana la ukanda wa soka wa Afrika mashariki na kati (Cecafa) baada ya kuifunga Kenya kwa mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliofanyika katika uwanja wa Kmc Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Pamoja na kupoteza mchezo huo Kenya imeungana na Tanzania kufuzu michuano ya Afcon 2025 itakayofanyika mwakani.

Ngorongoro Heroes walianza kufungwa dakika ya 47 lakini walisawazisha dakika ya 64 ya mchezo kwa bao la Valentino Mashaka aliyepokea pasi nzuri ya Shekhan Ibrahim huku Shekhan tena akifunga bao la ushindi dakika ya 82 kwa shuti kali baada ya beki wa Kenya kuokoa vibaya na mpira kumkuta mfungaji.

Katika Mchezo huo vijana hao wa chini ya umri wa miaka 20 walizawadiwa fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni ishirini kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk Samia Suluhu Hassan ikiwa ni pongezi kwa ushindi huo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala