Saturday, May 10, 2025
Home Soka Mamelod Sundowns Yatwaa AFL

Mamelod Sundowns Yatwaa AFL

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya soka ya Mamelod Sundowns imefanikiwa kuweka rekodi ya kutwaa taji la African Football League ikiwa ni mara ya kwanza michuano hiyo kufanyika baada ya kuifunga Wydad Athletic Club kwa mabao 2-1 katika mchezo wa fainali wa pili uliofanyika nchini Afrika ya kusini.

Katika mchezo wa kwanza nchini Morroco Mamelod ilikubali kipigo cha mabao 2-1 hivyo kuwalazimu kushinda katika mchezo wa fainali ya pili ambapo walihitaji ushindi wa aina yeyote ili kufuzu na hatimaye mabao mawili ya Peter Shalulile dakika ya 45′ na Aubrey Modiba dakika ya 53′ yalitosha kuipa ushindi Mamelod katika michuano hiyo mipya.

Katika mchezo huo wa Fainali uliofanyika katika uwanja wa Loftus Versfeld Rais wa Fifa Gian Infantino na Rais wa Caf Patrice Motsepe walihudhuria sambamba na viongozi wa timu nane zilizoshiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza.

banner

Kwa upande wa tuo binafsi kipa wa Mamelod Sundowns  Ronwens Williams alitwaa tuzo ya kipa bora huku Taphelo Maseko akitwa tuzo ya mchezaji bora sambamba na mfungaji bora huku tuzo ya mashabiki bora ikienda kwa mashabiki wa klabu ya Simba sc.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.