Klabu ya Arsenal imemsajiri na kumtambulisha rasmi kiungo fundi Albert Sambi Lokonga kutoka klabu ya Anderlecht ya Ubelgiji kwa mkataba wa mrefu kwa ada inayokadiriwa kufikia paundi milioni 17.
Mchezaji huyo alikuwepo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ubelgiji kwenye michuano ya Euro 2020 iliyomalizika hivi karibuni.
Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amesema ”Albert ni mchezaji mwerevu ameonesha ukomavu mkubwa.Amefundishwa soka na Vicent Kompany ambaye amekuwa akimzungumzia sana juu ya uwezo wake”.
Lokonga atavaa jezi namba 23 na tayari amejiunga na wachezaji wenzake wa Arsenal kwenye maandalizi ya msimu mpya.