Fei Toto Ajifunga Yanga sc

0

Kiungo Feisal Salum Fei toto amesaini mkataba mpya wa minne kuendelea kukipiga katika klabu ya Yanga sc ambapo atasalia klabuni hapo mpaka mwaka 2024.

Kiungo huyo kipenzi cha mashabiki wa klabu hiyo amesaini mkataba huo leo na kuzima tetesi za kutakiwa na klabu ya Simba sc ambazo zilikua zimezagaa.

Feisal amekua mmoja ya wachezaji tegemeo klabuni hapo huku pia akiwa na nidhamu ya hali ya juu ambayo imewafanya miamba hao kulazimika kumpa mkataba staa huyo.

Leave A Reply

Your email address will not be published.