Connect with us

Makala

Kibu Atambulishwa Rasmi Simba Sc

Baada ya kuripotiwa kuwa ameongeza mkataba wa kuendelea kusalia katika klabu ya Simba Sc,Sasa ni rasmi mshambuliaji Kibu Dennis ataendelea kusalia klabuni hapo kwa miaka miwili baada ya kutambulishwa rasmi na klabu hiyo.

Kibu amesaini mkataba huo wa miaka miwili ambapo atakaa klabuni hapo mpaka mwaka 2026 pindi mkataba huo utakapoisha huku akidaiwa kuvuta kiasi cha shilingi milioni mia tatu na gari ya kutembelea kwa miaka hiyo miwili atakayotumikia mkataba huo.

Pia mshahara wa staa huyo na Bonasi vimeboreshwa mara dufu kushinds mkataba wa awali aliousaini wakati anajiunga na klabu hiyo miaka miwili iliyopita akitokea klabu ya Mbeya City Fc.

Staa huyo kwa sasa yupo nchini Marekani katika mapumziko akisubiri kurudi nchini kwa ajili ya msimu mpya huku akiuguza jeraha la enka alilolipata katika michezo ya ligi kuu nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala