Connect with us

Soka

Gadiel Arejea Taifa Stars

Beki wa klabu ya Cape Town Spurs ya nchini Afrika ya kusini Gadiel Michael Mbaga baada ya kukiwasha katika Klabu yake hiyo hatimaye amejumuishwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kinachokwenda kushiriki michuano ya kirafiki nchini Saudi Arabia.

Gadiel Michael ilikua ni kama karia yake ya mpira imekwisha baada ya kuzitumikia Azam,Yanga na Simba lakini ni dhahiri kwamba benchi la unyamani ndilo lililokua linataka kumaliza maisha yake ya mpira.

Hata hivyo punde tu baada ya kujiunga na Singida Big Stars mwalimu Ernst Middendorp alimhamishie eneo la kiungo na kisha kumpa nafasi ya kutosha na baada ya kocha huyo kuachana na klabu hiyo na kuajiriwa na Cape Town City Spurs mara moja alimsajili mchezaji huyo na kumpa nafasi mara kwa mara ya kucheza.

Gadiel mpaka sasa ameitumikia klabu hiyo michezo takribani kumi tangu ajiunge kwa mkopo mwezi Januari mwaka huu na kufanikiwa kufunga bao moja na kutoa assisti mbili za mabao akicheza zaidi upande wa kushoto kama beki ama winga.

Beki huyo amerejea rasmi katika kikosi hicho cha Taifa Stars ambacho kesho atakwea pipa kwenda nchini Saudi Arabia kucheza michezo miwili ya kirafiki na timu ya Taifa ya Sudan.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka