Thursday, May 8, 2025
Home Makala Fountain Gate Fc Yaibamiza Kmc

Fountain Gate Fc Yaibamiza Kmc

by Sports Leo
0 comments

Timu ya Fountain Gate Fc imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Klabu ya Kmc Fc katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa uliopo mjini Babati.

Fountain Gate ilianza mchezo vizuri na kufanikiwa kupata bao la mapema dakika ya 8 ya mchezo likifungwa na Dickson Ambundo kutokana na makosa ya walinzi wa Kmc.

Selemani Mwalimu Gomez ambaye ni mchezaji bora wa ligi kuu ya Nbc kwa mwezi Septemba alifunga bao la pili kwa wenyeji dakika ya 23 ya mchezo ambapo pia katika mchezo huo alikabidhiwa tuzo yake ya mchezaji bora wa mwezi Septemba.

banner

Kmc pamoja na jitihada zao za kusawazisha walijikuta wakiishiwa nguvu baada ya mshambuliaji wao Ibrahim Elias kupewa kadi nyekundu kutokana na mchezo mbaya ambapo hali hiyo iliwapunguza nguvu na kujikuta wanaruhusu bao la tatu dakika ya 59 likifungwa na William Edgar kwa shuti kali.

Kmc walipata bao la kufutia machozi likifungwa na Andrew Vicent Dante dakika ya 47 akiunganisha vyema mpira wa faulo uliokua unazagaa langoni mwa Fountain Gate Fc.

Kutokana na ushindi huo sasa Fountain Gate Fc imefikisha alama 16 katika michezo nane ya ligi kuu ya Nbc ikiwa katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kuu huku Kmc ikiwa katika nafasi ya 10 ya msimamo ikiwa na alama 8 katika michezo 8 ya ligi kuu ya Nbc.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.