Mshambuliaji kinara wa klabu ya Azam Fc Prince Dube, amefanikiwa kuchaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi Mei mwaka huu, wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
Dube ametwaa tuzo hiyo baada ya kuonyesha kiwango bora kabisa katika mechi za mwezi huo, akifunga mabao mawili katika mechi mbili na kuisaidia Azam FC kuvuna pointi kiasi cha kuanza kutikisa nafasi ya pili ya ligi ambayo inamilikwa na Yanga sc.
Pia kocha mkuu wa klabu hiyo George Lwandamina nae ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwezi pamoja na meneja wa uwanja wa Azam Complex anayefahamika kwa jina la sikitu ameibuka meneja bora wa uwanja wa mwezi Mei.