Tuesday, May 6, 2025
Home Soka Agrey Arejea Mdogomdogo Azam fc

Agrey Arejea Mdogomdogo Azam fc

by Sports Leo
0 comments

Beki kisiki wa klabu ya Azam fc na timu ya taifa ya Tanzania Aggrey Morris ameanza mazoezi ya viungo ili kujiweka fiti baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu tangu aumie akiwa na timu ya taifa(Taifa stars).

Agrey aliumia katika kambi ya taifa stars iliyokua nchini Misri kujiandaa na michuano ya mataifa ya Afrika(Afcon 2019) ambapo aliumia wakati wa mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na michuano hiyo dhidi ya Misri na tangu hapo amekua nje ya uwanja kutokana na maumivu hayo ya goti.

Beki huyo ni mmoja ya mabeki bora na wakongwe nchini ambapo amefanikiwa kudumu na kiwango kile kile kwa muda mrefu na kurejea kwake ni faraja kwa klabu yake ya Azam fc.

banner

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.