Alcantara Atua Liverpool

0

Kiungo wa klabu ya Bayern Munchen Thiago Alcantara amekamilisha usajili wake kutua katika klabu ya Liverpool ya ligi kuu nchini Uingereza.

Uhamisho huo umeigharimu Liverpool kiasi cha Paundi Milioni 27 huku kukiwa na nyongeza mbalimbali endapo mchezaji huyo atakua na mchango mkubwa klabuni hapo.

Awali kiungo huyo alihusishwa na timu za Manchester United na Paris st.German lakini Jurgen Klopp amefanya kazi ya ziada kuhakikisha kiungo huyo anatua klabuni hapo licha ya kukabiliwa na ushindani mkali.

Leave A Reply

Your email address will not be published.