Connect with us

Makala

Kiduku Kukipiga J’mosi

Bondia Twaha Kiduku anatarajiwa kupanda ulingoni siku ya Jumamosi kuzichapa na Alex Kabangu katika pambano la uzito wa kati la kuwania ubingwa wa UBo litakalofanyika mkoani morogoro.

Pambano hilo la raundi nane litafanyika mkoani Morogoro ambako ni nyumbani kwa kina Kiduku ambapo viingilio vitakua ni elfu 10 na ishirini huku upande wa viti maalumu itakua elfu 30.

Mratibu wa pambano hilo, Bakari Khatibu amesema kuwa maandalizi ya pambano yamekamilika kwa asilimia 100 huku akiwataka wadau wangumi nchini kujitokeza kwa wingi kushuhudia pambano hilo.

“Maandalizi kwa upande wetu ni mazuri tunashukuru Mungu tayari Kabangu ameshaingia na yupo hapa Morogoro, tunachosubiria ni siku kufika kwa ajili ya mambo mengine”.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala