Connect with us

Makala

Yanga Sc Haishikiki Nbc

Haishikiki na wala haikamatiki,Ndio unavyoweza kusema kutokana na mfululizo wa ushindi inaopata klabu ya Yanga sc katika michuano ya ligi kuu ya Nbc nchini baada ya kuibamiza Pamba Jiji Fc kwa mabao 3-0 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Ccm Kirumba jijini Mwanza.

Ikianza bila mastaa wake Stephan Aziz Ki,Pacome Zouzoua,Dickson Job na Cletous Chama,Iliwachukua takribani dakika 26 kupata bao la uongozi kupitia faulo iliyopigwa kiufundi na Chadrack Boka na kumuacha kipa Yona Amos akishangaa.

Pamba Jiji Fc waliocheza kwa kujituma walikosa nafasi kadhaa kupitia kwa mshambuliaji mkenya Tegisi Momanyi huku pia wakikosa utulivu eneo la kiungo.

Kipindi cha pili kocha Miloud Hamdi alimuingiza Stephan Aziz Ki kuchukua nafasi ya Khalid Aucho aliyepumzishwa kutokana na kuwa na mechi dhidi ya Simba Sc wiki ijayo.

Azizi Ki aliingia na kufunga mabao mawili ya haraka haraka akiunganisha kwa kichwa krosi ya Maxi Nzengeli na kufunga dakika ya 75 huku dakika mbili baadae alifunga kwa shuti la mbali akimdhidi maarifa kipa Yona Amos.

Mpaka dakika tisini zinamalizika Yanga sc walifanikiwa kuchukua alama tatu na kufikisha alama 58 kileleni mwa ligi kuu wakiwa na michezo 22 huku Pamba jiji wakisalia katika nafasi ya 13 wakiwa na alama 22 katika michezo 22 ya ligi kuu ya Nbc nchini.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala