Sunday, May 11, 2025
Home Makala U23 Yafuzu kwa Mbinde

U23 Yafuzu kwa Mbinde

by Sports Leo
0 comments

Timu ya Taifa ya Vijana chini ya Umri wa miaka 23 imefanikiwa kufuzu hatua inayofuatia ya kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya mataifa ya Afrika  itakayofanyika mwakani nchini Morroco baada ya kupata sare ya 3-3 katika mchezo wa marudiano dhidi ya Sudan Kusini uliofanyika jijini Kigali nchini Rwanda.

Kutokana na sare hiyo Stars U23 inafuzu kutokana na faida ya bao la ugenini baada ya kutoka suluhu katika mchezo wa hapa nyumbani siku ya Ijumaa Septemba 23 ambapo licha Stars kuwa na mastaa wengi wa ligi kuu nchini bado haikufua dafu kwa Wasudan hao.

Vijana wa Stars walikua wa kwanza kuandika bao dakika ya 10 likifungwa na Abdul Sopu kwa penati baada ya Kelvin John kuangushwa katika eneo la hatari japo bao hilo lilisawazishwa dakika ya 25 na Dani Thon 25′ na Stars ikafanikiwa kupata bao la pili dakika ya Ally Msengi 40′ ambalo lilisawazishwa na Joseph Manase 53′ na Sudan wakafanikiwa kupata bao la tatu kupitia kwa Rehan Malong 66′ kwa penati lakini baada ya dakika moja Stars walisawazisha kupitia kwa Kelvin John na matokeo yalisalia hivyo hivyo mpaka dakika ya mwisho.

banner

Stars u23 kwanza inatakiwa kuongeza bidii na mbinu katika hatua inayofutia ambapo itakutana na Nigeria U23 ambapo mshindi ndio atakata tiketi ya kufuzu kwenda katika fainali hizo zitakazofanyika mwezi juni mwakani nchini Morroco.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.