Connect with us

Makala

Tajiri Chelsea Akubali Yaishe

Tajiri wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich amekubali kuuzwa kwa klabu ya Chelsea huku Serikali ya Uingereza ikisimamia kila kitu ikiwemo kuchukua faida ya uuzwaji wa timu hiyo inayofanya vizuri nchini humo.

Awali baada ya Urusi Kuivamia Ukraine mataifa ya Nato ambayo Uingereza ni mwanachama yaliiwekea vikwazo vya kiuchumi serikali ya Urusi chini ya Vladimir Putin ikiwemo kuzuia mali zote za matajiri wa kirusi nchini humo ambapo klabu ya Chelsea imeathirika kutokana na mmiliki wake kuwa Mrusi huku akitajwa kuwa rafiki wa karibu wa Putin.

Akaunti za klabu hiyo tayari zimefungwa huku wakiruhusiwa kufanya shughuli chache za soka chini ya usimamizi wa serikali ya Uingereza ambao pia walizuia kuuzwa kwa klabu hiyo lakini uamuzi wa bilionea huyo kuruhusu kukabidhidi usimamizi wa uuzwaji kumilikiwa na serikali imekua ahueni kwa klabu hiyo kuendelea na mchakato wa uuzwaji.

Chelsea ipo katika nafasi ya tatu ya msimamo wa Epl ambapo imepitwa na kinara Man city kwa alama 13 huku ikikazana angalau kumaliza katika nne bora ili kupata kushiriki michuano ya Uefa mwakani.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala