Connect with us

Makala

Singida Black Stars Yamtangaza Ouma Kocha Mkuu

Klabu ya Singida Black Stars imetangaza kuwa sasa itakuwa chini ya kocha David Ouma kama Kocha mkuu na  Muhibu Kanu kama kocha msaidizi wa klabu hiyo wakichukua nafasi ya Miloud Hamdi.

Hii inakuja baada ya aliyekuwa kocha wao mkuu Miloud Hamdi kutimkia kunako klabu ya Yanga kuchukua nafasi ya kocha Sead Ramovic ambaye ameachana na wanajangwani hao.

David Ouma aliwahi kuwa kocha wa Coastal Union kabla ya kutemana nao ambapo sasa atakua na jukumu hilo zito la kuhakikisha klabu hiyo inafanya vizuri katika ligi kuu nchini.

Mpaka sasa katika msimamo wa ligi kuu Singida Black Stars ipo nafasi ya nne ya msimamo wa ligi kuu na inatarajiwa kuwa na mchezo dhidi ya timu ya Kagera Sugar Fc katika uwanja wa Liti mjini Singida.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala