Klabu ya Simba sc imeondoshwa katika michuano ya Mapinduzi Cup inayoendelea huko Zanzibar baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 katika mchezo wa kwanza dhidi ya Mlandege Fc uliofanyika katika uwanja wa Amaan Visiwani Zanzibar.
Simba sc ikianza na idadi kubwa ya mastaa wanakalia benchi kama vile Nassoro Kapama,Kennedy Juma,Gadiel Michael,Kibu Dennis,Habib Kyombo na wengineo ilishindwa kuwa na muunganiko mzuri hasa eneo la kati lililokua chini ya Nelson Okwa na Jonas Mkude.
Dakika ya 75 Mlandege ilipata Bao la ushindi kwenye mchezo huo lilifungwa na Abubakar Mwadin kutokana na makosa ya ulinzi wa nyota wa Simba kuanzia kwa mabeki ambao hawakuruka vizuri na kumuacha Beno Kakolanya akiwa hana la kufanya.
Kutokana na Matokeo hayo sasa Mlandege Fc imefikisha alama nne kileleni mwa kundi C huku mchezo kati ya Simba sc na Kvz ukiwa ni wa kukamilisha ratiba tu maana tayari Mlandege amefuzu hatua ya nusu fainali.