Connect with us

Makala

Simba sc Yapaa Uturuki

Kikosi cha Simba sc kimeondoka nchini jioni ya tarehe 11/7/2023 kuelekea nchini Uturuki kwa kambi ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu na michuano ya kimataifa ambayo klabu hiyo itashiriki kuanzia msimu ujao.

Kambi hiyo muhimu kwa maandalizi ya utimamu wa mwili na kutengeneza muunganiko wa kikosi hicho ambacho mpaka sasa kimesajili mastaa takribani wanne  huku pia ikiwa na benchi jipya la ufundi chini ya mkufunzi Roberto Oliveira.

Mastaa kama Andre Onana,Aubin Kramo,Che Fondoh Malone,David Kameta watapata nafasi ya kufundishwa mbinu mpya za mwalimu Robertinho huku pia wakiangaliwa jinsi ya kutengeneza muunganiko mzuri na mastaa kama Cletous Chama na Saido Ntibanzokiza ambao kwa muda mfupi wamejenga ufalme klabuni hapo.

Katika msafara huo mbali na wachezaji pia baadhi ya watalaamu wapya wa benchi la ufundi la klabu hiyo waliotambulishwa siku chache zilizopita pia wameambatana na klabu hiyo tayari kuanza kuingiza utaalamu wao kikosini humo.

Simba sc mapema mwanzoni mwa mwezi Augusti italazimika kucheza michuano ya ngao ya hisani dhidi ya Singida Fountain Gate ambapo ikishinda itakutana na mshindi kati ya Yanga sc na Azam Fc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala