Connect with us

Makala

Yanga sc Yawasili Ethiopia

Msafara wa kikosi cha Timu ya Yanga sc umefanikiwa kuwasili salama nchini Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa raundi ya pili ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Cbe SA utakaofanyika siku ya Jumamosi Septemba 14 mwaka huu.

Msafara huo ulianza safari mapema alfajiri ya leo ukiwa na baadhi ya mastaa wa kikosi cha kwanza huku wengine wataungana na kikosi moja kwa moja nchini humo wakitokea katika timu zao za Taifa zilizokua na michezo ya kujiandaa na michuano ya mataifa ya Afrika mwaka 2025 yatakayofanyika nchini Morocco.
6

Msafara huo wa Yanga sc utakutana na mastaa kama Stephane Aziz Ki,Duke Abuya,Prince Dube,Djigui Diarra sambamba na Cletous Chama na Kennedy Musonda ambao watatokea nchini mbalimbali kulingana na ratiba za michezo ya timu zao za Taifa.

Yanga sc inavaana na Cbe SA katika raundi ya pili baada ya kufanikiwa kuwafunga Vital O ya nchini Burundi kwa jumla ya mabao 10-0 katika michezo miwili ya raundi ya awali.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala