Friday, May 9, 2025
Home Makala Simba sc Ndio Basi Tena

Simba sc Ndio Basi Tena

by Sports Leo
0 comments

Matokeo ya sare ya 1-1 waliyopata klabu ya Simba sc katika mchezo wa ligi kuu nchini dhidi ya Geita Gold Fc yamezidi kufifisha matumaini ya ubingwa wa ligi kuu kwa msimu huu baada ya kushindwa kupunguza pengo la alama baina yake na Klabu ya Yanga sc ambayo iko kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini.

Simba sc ilipata sare hiyo katika mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Ccm Kirumba huku wakilazimika kusawazisha goli la George Mpole aliyefunga dakika ya 24 huku Kibu Dennis aliyesawazisha kwa kichwa akiunganisha kona ya Rally Bwallya.

Simba sc sasa imefikisha alama 51 nyuma ya Yanga sc yenye alama 63 katika michezo 25 ya ligi kuu nchini ambapo Yanga sc inahitaji alama nne pekee katika michezo mitano ili kutwaa ubingwa wa 28 wa ligi kuu nchini.

banner

Ili Simba sc itwae ubingwa msimu huu inabidi Yanga sc wapoteze michezo yote mitano ama wapate sare michezo mitatu na kufungwa minne huku Simba sc wakitakiwa kushinda michezo yote mitano iliyosalia kitu ambacho ni kigumu kutokea kutokana na aina ya kikosi cha Yanga sc.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.