Connect with us

Makala

Samatta ,Tanzania Itanipa Sapoti

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samatta anayekipiga Klabu ya Aston Villa amesema kuwa uwepo wake Aston Villa ataungwa mkono na watanzania wengi kwani ni mtanzania wa kwanza kucheza ligi kuu England.

“Ilikuwa ni maombi yangu ya muda mrefu na ndoto zangu kucheza Ligi Kuu ya England  tangu nikiwa mdogo nilikuwa nikiitazama ligi hii kwenye TV na Aston Villa ni miongoni mwa timu nilizokuwa nazitama hivyo Kuja kwangu hapa ninaamini nitapewa sapoti na mashabiki wangu wa Tanzania”alisema Samatta

Aston Villa leo itakuwa na kibarua mbele ya Leicester City wakiwa nyumbani ikiwa ni mchezo wa marudio, Kocha Mkuu wa Villa Dean Smith amesema kuwa Samatta anaweza kuanza leo kwani  wanatakiwa kushinda ili kusonga mbele baada ya mchezo wa Kwanza kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala