Connect with us

Makala

Saido Alamba Pesa nene Simba sc

Staa wa zamani wa klabu ya Yanga sc Saido Ntibanzokiza amelamba dili la mkataba mnono wa kujiunga na klabu ya Simba sc kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu ambapo mkataba huo amelamba pesa nono kutoka kwa matajiri hao wa kariakoo.

Katika mkataba huo staa huyo amelamba pesa ya usajili kiasi cha zaidi ya milioni 60 za kitanzania pamoja na mshahara wa dola za kigeni elfu nne ambao ni zaidi ya milioni tisa za kitanzania huku pia akipewa nyumba maeneo ya masaki ama Oysterbay na mikocheni kulingana na eneo itakapopatikana kwa urahisi zaidi.

Licha ya kutambulishwa staa huyo pamoja na kuhudhuria mazoezi bado hajacheza mchezo wowote mpaka sasa huku pia akiwekewa masharti mazito kuhusu masuala ya nidhamu ikiwemo kukatwa pesa endapo atafanya utovu wowote wa nidhamu baada ya taarifa za Yanga sc kuwa alikua msumbufu mara kadhaa.

Staa huyo kutoka Burundi alijiunga na Geita Gold sc akitokea Yanga  sc ambapo mpaka sasa anajiunga na Simba sc alikua amefanikiwa kutoa assisti sita na kufunga mabao matatu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala