Connect with us

Makala

Yanga sc Yajichimbia Kileleni

Klabu ya Yanga sc imeendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini baada ya kufanikiwa kuwafunga Azam Fc kwa mabao 3-2 katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

Azam Fc ilianza kupata bao la mapema dakika ya 27 likifungwa na Abdul Sopu lakini bao hilo halikudumu kwa Fiston Mayele alisawazisha dakika ya 31 kisha dakika ya 33 Aziz Ki aliwafungia Yanga sc bao la pili akiunganisha pasi ya Mayele ambapo matokeo hayo yalidumu mpaka wakati wa mapumziko.

Azam fc mapema dakika ya 47 Abdul Sopu alifunga tena bao la kusawazisha akiunganisha pasi ya Kipre Junior na bao hilo lilifanya mchezo uwe mkali na kushambuliana kwa zamu mpaka pale mwalimu Nabi alimtoa Morrison na Moloko na kuwaingiza Kisinda na Farid Musa ambaye alifunga bao la tatu dakika ya 78 bao ambalo lilidumu mpaka dakika 90 za mchezo.

Yanga sc baada ya ushindi huo iliendelea kuzima ndoto za Azam Fc za kumaliza wakiwa mabingwa baada ya kuwaacha kwa alama 11 wakiwa na alama 47 kileleni huku Azam Fc wakiwa na alama 37 wote wakiwa wamecheza michezo 18 ya ligi kuu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala