Friday, May 9, 2025
Home Makala Msuva Mbioni Kujiunga Yanga sc

Msuva Mbioni Kujiunga Yanga sc

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji Simon Msuva yupo katika hatua za mwisho kujiunga na klabu ya Yanga sc katika usajili wa dirisha dogo baada ya kuachana na klabu yake ya Js Kybilie ya nchini Algeria kwa makubaliano ya pande mbili.

Mpaka sasa mazungumzo baina ya mabosi wa klabu hiyo na Yanga sc yamefikia hatua nzuri kutokana na klabu hiyo kumuwekea dau nono na mshahara mkubwa kuja kujiunga na mastaa Aziz Ki,Pacome Zouzou kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo.

Pamoja na Msuva pia klabu hiyo inaangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji Karamoko Sankara kutoka Asec Mimosa huku ikiwa na mpango wa kuachana na Gift Fred na Hafiz Konkoni kutokana na kushindwa kumshawishi mwalimu Miguel Gamond.

banner

Msuva bado ana nia ya kucheza nje ya Tanzania lakini kutokana na ushawishi wa mabosi wa Yanga sc anafikiria kukubali dili hilo ambapo anasubiri kushauriana na familia yake kwa mara ya mwisho ndio atatoa uamuzi.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.