Connect with us

Makala

Mshery Kufanyiwa Upasuaji

Klabu ya Yanga sc imeamua kumpeleka nchini Morroco golikipa wake namba mbili AbouTwalib Mshery ambaye anasumbuliwa na goti ili apone haraka ambapo atafanyiwa upasuaji na wataalamu wabobezi wa masuala ya viungo.

Maamuzi hayo yamefikiwa kutokana na umuhimu wa kipa huyo wakati klabu hiyo ikielekea katika michuano ya kimataifa ambapo mpaka sasa inao makipa wengine watatu wakiongzowa na Djigui Diarra,Metacha Mnata ambaye yupo kwa mkopo wa miezi sita na Erick Johora.

Wataalamu hao ambao watamfanyia matibabu kipa huyo ni wale ambao walimtibu Kibwana Shomari na Yacouba Songne ambao nao walikua wakisumbuliwa na magoti.

Mshery tangu asajiliwe Yanga sc amefanikiwa kuwa mbadala wa kudumu wa Djigui Diarra ambaye hata anapokosekana kinda huyo hufanya kazi nzuri inayowavutia mashabiki wa soka nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala