Mastaa wa klabu ya Yanga waliokua majeruhi Khalid Aucho, Pacome Zouzoua, Clatous Chama, Kennedy Musonda leo hii wamerejea mazoezini baada ya kupona majeraha yao.
Mbali na mastaa hao pia Yao Kouassi aliyekua na majeraha ya muda mrefu nae amerejea mazoezini licha ya kuwa hajaanza program za kufanya mazoezi na wenzake ndani ya uwanja.
Daktari wa klabu hiyo Moses Etutu amesema kuwa mastaa hao wamerejea baada ya kupona majeraha kabisa ambapo Pacome Zouzoua,Cletous Chama na Kennedy Musonda wapo tayari kuanza kutumika kama kocha akiwahitaji huku Yao Kouassi akiendelea na mazoezi ya kutafuta utimamu wa mwili.
“Kutokana na mchezo ujao kuwa zaidi ya siku saba mbele wachezaji hao wapo tayari kutumika isipokuwa Yao Kouassi ambaye tunaendelea na matibabu ya kumpatia utimamu wa mwili ili awe sawa kama wenzake”,Alisema Daktari huyo.
Yanga sc katika msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini wana alama 70 wakiwa kileleni huku wakisaliwa na michezo mitatu pekee.