Connect with us

Makala

Kuna Swali?

Ndivyo wanavyouliza mashabiki wa Simba sc baada ya kumaliza ule utata wa siku nyingi juu ya ubora wa kikosi chao baada ya kufanikiwa kuifunga Simba sc kwa mabao 2-0 katika mchezo mkali wa kusisimua wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

Simba sc ikianza bila kipa wake namba moja Aishi Manula na kiungo Sadio Kanoute ilipata bao la mapema kupitia kwa Henock Inonga dakika ya pili akiunganisha pasi safi ya Shomari Kapombe iliyotokana na kona.

Yanga sc walijitahidi kusawazisha bao hilo lakini walikosa nafasi kadhaa za wazi kupitia kwa Fiston Mayele na Kennedy Musonda hivyo kuzidi kujiweka katika mazingira magumu hasa baada ya Simba sc kupata bao la pili kupitia shuti kali la Kibu Dennis dakika ya 31 ambapo mabao hayo yalidumu mpaka wakati wa mapumziko.

Kocha Nabi licha ya kufanya mabadiliko kadhaa katika kipindi cha pili akiwaingia Mudathir Yahaya,Tuisila Kisinda na Stephane Aziz Ki lakini mabadiliko hayo hayakua na cha ziada mpaka dakika tisini zinakamilika bado ubao ulisomeka 2-0.

Kutokana na ushindi huo sasa Simba sc imepunguza pengo la alama kutoka nane mpaka tano ikiwa katika nafasi ya pili huku zikiwa imesalia takribani michezo minne ligi kufika mwishoni.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala