Kiungo anayekipiga ndani yaklabu ya Yanga,Feysal Salum’Feitoto’ ambaye pia ni miongoni mwa viungo anayemkubali Clatous Chama wa Simba Sc ameonesha nia ya kuibukia huko kwa masharti.
Fei Toto kwa sasa yupo zake Visiwani Zanzibar baada ya ligi kusimamishwa kutokana na janga la Virusi vya Corona ila amesema kuwa anaweza kucheza ndani ya klabu ya Simba iwapo viongozi wake watamruhusu kufanya hivyo kwani bado ana mkataba mrefu na Yanga lakini hana shida iwapo itatokea klabu ya Simba ama nyingine zikahitaji saini yake.
“Mimi ni mchezaji wa Yanga viongozi wananipenda nami nawapenda pia ikitokea klabu inahitaji saini yangu utaratibu ufuatwe sina hiyana nitasaini bila tatizo,” alisema Feitoto