Home Makala Karia Awatembelea Serengeti U23

Karia Awatembelea Serengeti U23

by Sports Leo
0 comments

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia ametembelea kambi ya Timu ya Taifa ya wanaume U23 kuelekea mchezo wa kufuzu AFCON dhidi ya Nigeria utakaochezwa kesho Oktoba 22, 2022 uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Serengeti U23 wanawania kufuzu fainali za michuano ya mataifa ya Afrika mwakani nchini Morroco ambapo wanalazimika kukutana na Nigeria baada ya kufanikiwa kuwatoa Sudan Kusini kwa jumla ya mabao 3-3 baada ya awali kutoa suluhu katika mchezo wa hapa nyumbani uliofanyika uwanja wa Chamazi jijini Dar es salaam.

Baada ya mchezo huo dhidi ya timu hiyo ya Nigeria U23 iliyojaa mastaa wanaocheza ulaya kikosi hicho kitajiandaa na safari ya kwenda nchini Nigeria kwa mchezo wa marudiano utakaofanyika wiki ijayo Oktoba 28 ambapo mshindi wa jumla ndio atawakilisha katika michuano hiyo ya Afcon kwa vijana wa umri wa miaka 23 inayofanyika nchini Morroco.

banner

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.