Connect with us

Makala

Man Utd Yaibukia kwa Liverpool

Klabu ya Manchester united chini ya kocha Erick Ten Hag imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Liverpool fc katika mchezo wa mzunguko wa tatu wa ligi kuu nchini Uingereza uliofanyika katika uwanja wa Old Trafford jijini Manchester.

Iliwachukua Man united dakika 16 kuandika bao la kwanza la kideo ambapo Jadon Sancho alimpiga chenga kali James Milner na kuandika bao la kwanza kwa United huku bao hilo lilidumu mpaka kipindi cha pili ambapo Marcus Rashford aliwahadaa mabeki na kupata bao la pili dakika ya 64.

Ikiwa bila nahodha Harry Maguire na Cristiano Ronaldo United ilijitahidi kukumbia uwanjani kuwabana Liverpool waliokua na washambuliaji hatari wakiongozwa na Mohamed Salah ambao walipata bao la kwanza dakika ya 81 lakini mpaka dakika 90 zinamalizika Man united iliondoka na alama tatu.

Manchester United ambayo ilipoteza michezo miwili ya mwanzo sasa imefikisha alama 3 na kukaa katika nafasi ya 14 huku Liverpool wakiwa katika nafasi ya 16 wakiwa na alama 2.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Makala