Connect with us

Makala

Kaizer Chiefs Yakomaa na Diarra

Klabu ya Kaizer Chief ya Afrika Kusini Imefungua mlango wa mazungumzo na Uongozi wa klabu ya Yanga sc ya Tanzania kuona kama wanaweza kumpata Mlinda lango huyo bora kwenye dirisha kubwa la usajili.

Kaizer chiefs hawajaridhishwa na ubora wa magolikipa wao wawili raia wa Rwanda Fiacre Ntwari na Raia wa Afrika kusini Bruce Bvuma walioruhusu mabao 24 kwenye michezo 20 ya ligi kuu.

Kocha Nasredine Mohamed Nabi anataka kuhakikisha kuwa kikosi chake kinapambana kumpata golikipa huyo mzoefu wa soka barani Afrika ambapo mpaka sasa Pamoja na klabu hiyo kutuma ofa bado haijajibiwa na klabu yake ya Yanga Sc.

Diarra mwishoni mwa msimu uliopita aliongeza mkataba wa miaka mitatu na klabu yake ya Yanga sc kuendelea kuitumikia klabu hiyo hivyo Kaizer Chiefs inapaswa kutoa fedha ndefu kumnasa kipa huyo aliyetokea kuwa kipenzi cha mashabiki wa klabu hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala