Connect with us

Makala

Bongo Zozo Atua Lipuli Fc

Uongozi wa Timu ya Lipuli FC ya mkoani Iringa imemtangaza shabiki na mhamasishaji wa Timu ya taifa ya Tanzania Nick Reynolds maarufu kama Bongo zozo kuwa Balozi wake kwa lengo la kuitangaza timu ya Lipuli FC pamoja na kusaidia wachezaji wake kucheza Kimataifa.

“Nimependa na nitaenda kufanya kazi, nitasafisha njia ili wachezaji wawe na uwezo wa kuonesha utaalamu wao, unaweza kuwa mchezaji mzuri sana lakini Waingereza hawakujui lakini mimi nitasafisha njia”, amesema Bongo Zozo.

Bongo zozo amesaini mkataba huo mbele ya waandishi wa habari makao makuu ya klabu hiyo mkoani Iringa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala