Wednesday, May 7, 2025
Home Makala Azam Fc Watimua Kocha

Azam Fc Watimua Kocha

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Azam Fc imeamua kuachana na kocha Dennis Lavigne ambaye ilimsajili wiki chache zilizopita kutokana na kuwa na mfululizo wa matokeo mabaya sambamba na kutoelewana na baadhi ya mastaa wa klabu hiyo hasa wale wa kikosi cha kwanza.

Kutimuliwa kwa kocha huyo Mfaransa kumechagizwa na kipigo cha mabao 2-1 ilichokipata klabu hiyo kutoka kwa Kmc katika mchezo wa ligi kuu siku ya ijumaa na kufikisha alama 11 katika michezo saba ya ligi kuu msimu huu.

Azam Fc ilibadili benchi la ufundi kwa kumuondoa Ahmid Moallin na kuwaleta Lavagne na wasaidizi wake akiwemo kocha wa viungo na kocha wa washambuliaji ambaye ni Kally Ongala kwa lengo la kuleta mabadiliko kikosini ili kufanya vizuri katika msimu huu wa ligi kuu ambapo pia baadhi ya mastaa wapya walisajiliwa akiwemo Tape Edinho,James Akaminko na wengineo.

banner

Lavagne ambaye ameiongoza Azam Fc katika mechi sita akishinda tatu nakupoteza tatu ameondolewa klabuni hapo na nafasi yake itakaimiwa na Kally Ongala sambamba na Aggrey Morris mpaka pale itakapotangazwa vinginevyo na uongozi wa klabu hiyo.

 

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.