Taarifa za vyombo vya usalama nchini Marekani zinasema kuwa waliofariki mpaka jana katika ajali ya helikopta iliyotokea jana huko Los Angeles Marekani wamefika saba ambao ni Kobe Bryant, mwanaye Gianna Maria Onore, rafiki wa mwanaye, Alyssa ambaye aliambatana na wazazi wake John Altobelli na Keri.
Kocha wa Gianna na Alyssa kwenye kituo cha kufundisha mchezo wa mpira wa kikapu cha Kobe anayefahamika kama Christina Mauser na abiria wengine ni Sarah, Payton Chester na rubani Ara Zobayan.
Maelfu ya watu wamefurika nje ya uwanja wa nyumbani wa Los Angeles Lakers, Staples Center muda mfupi baada ya kutokea kwa kifo hicho kila mmoja akimuenzi Kobe Bryant na mwanae kwa namna yake.
Katika kituo cha Mamba Sports Academy wachezaji watoto wote walikuwa wakisubiri kocha wao mlezi Christina Mauser na kocha mkuu Kobe Bryant waje na wachezaji wawili ambao ni Gianna na Alyssa kwa ajili ya mchezo uliokuwa unafuata.
Bahati mbaya ni kuwa badala ya kufika wao zikafika taarifa za msiba wa ndugu zao na kwa pamoja walipiga magoti kwa pamoja wakiwaombea ndugu zao wapumzike kwa amani huku mmiliki wa timu ya Dallas, Mavericks Mark amesema timu yake itastaafisha jezi namba 24 kwa heshima ya Kobe.