Connect with us

Makala

Fadlu Ahitajika Morocco

Kwa mujibu wa ripoti kutoka nchini Morocco zinaeleza kuwa klabu ya FAR Rabat ya nchini humo imetuma ofa kwenda klabu ya Simba kwaajili ya kuihitaji saini ya kocha wa klabu ya Simba Fadlu Davies.

FAR Rabat imemtimua kocha wake Hubert Velud na wanahitaji kocha mwingine ambaye ataiongoza klabu hiyo kufikia malengo yao na Fadlu ndiye lengo lao kubwa kwa sasa.

Hata hivyo klabu hiyo itakua na kazi kubwa ya kufanya ili kumnasa kocha huyo kutokana  na kuwa na mkataba na klabu hiyo aliyojiunga nayo msimu huu.

Pia pamoja na hilo FAR Rabat watapata wakati mgumu kutokana na kocha huyo kuwa na project ndefu na klabu hiyo ya kuirudisha katika makali yake baada ya kukosa ubingwa kwa takribani misimu mitatu.

Fadlu amefanikiwa kuirudisha Simba Sc katika makali yake ambapo kwanza imekua na soka la kuvutia huku ikipata alama katika michezo ya ndani na nje ya nchi kiasi cha kufanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala