Klabu ya Yanga sc imepangwa katika kundi gumu la michuano ya klabu bingwa barani Afrika ambapo imepangwa kundi B sambamba na timu za Al Hilal Fc ya nchini Sudan,Tp Mazembe ya nchini Congo Dr sambamba na klabu ya Mc Algers ya nchini Algeria.
Yanga sc ina kazi ya ziada kupambana kuvuka kundi hilo ambalo linaonekana ni kundi la kifo kutokana na aina ya timu zilizomo katika kundi hilo ambazo nyingi zimewahi kuchukua ubingwa wa michuano hiyo kama Al Hilal Fc na Tp Mazembe japo kwa sasa hazina ubora kama ilivyokua zamani huku Yanga sc ikiwa imepandisha ubora kwa kiwango kikubwa sana.
Yanga sc itaanzia nyumbani na kisha dhidi ya Al Hilal Fc Novemba 27 mwaka huu na kumalizia pia nyumbani mwezi Januari mwakani dhidi ya Mc Algers ya Algeria.
Yanga sc inapaswa kuhakikisha kwanza inashinda michezo yake ya nyumbani ili kujitengenezea nafasi ya kufuzu ambapo itapata alama tisa huku ugenini ijitahidi kupata sare ili kufikisha alama kumi ambazo bila shaka zitaitosha kuvuka hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika kwa ngazi za klabu.
Msimu uliopita Yanga sc ilishindwa kuingia hatua ya nusu fainali baada ya kutolewa kwa matuta na Klabu ya Mamelod Sundowns baada ya kutoka suluhu michezo yote miwili ndani ya dakika 180 za nyumbani na ugenini.