Tuesday, May 6, 2025
Home Soka Yanga Sc “Out” Mapinduzi Cup

Yanga Sc “Out” Mapinduzi Cup

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga sc imetolewa nje ya michuano ya Maponduzi Cup baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa APR mchezo uliofanyika katika uwanja wa Amani Visiwani humo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa mashabiki wa klabu hiyo.

Kocha Miguel Gamond alionekana kutoupa uzito mchezo huo baada ya kuanza na wachezaji wengi wa kikosi B ambapo alichanganya na wale wa kikosi cha wakubwa kiasi kama vile Clement Mzize,Gift Fred,Mahalatse Makudubela,Farid Musaa na Kibwana Shomari na Jesus Moloko aliyefunga bao pekee la Yanga sc dakika ya 23 akipokea pasi ya clement Mzize.

APR walisawazisha bao hilo mwishoni mwa kipindi cha kwanza kupitia kwa Soulei Sanda na kipindi cha pili walifunga mabao mawili ikiwemo penati iliyofungwa na Mbaoma Victor dakika ya 49 huku Sharaf Shaiboub akifunga bao la mwisho dakika ya 79 na kuhitimisha kalamu ya mabao kwa timu hiyo.

banner

Yanga sc sasa inapaswa kurejea nchini baada ya kutolewa katika michuano hiyo huku mashabiki wengi wakilaumu benchi la ufundi kwa kuwajumuisha wachezaji wasio na uzoefu hasa katika mchezo huo wa robo fainali.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.