Friday, May 9, 2025
Home Makala Yanga sc Kukipiga na Kaizer Pre Seasons

Yanga sc Kukipiga na Kaizer Pre Seasons

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya  Yanga Sc imekubali ombi la Kaizer Chief kucheza mchezo wa Kirafiki wakati wa Pre Season ambapo mchezo huo utapigwa nchini Afrika Kusini mwezi Julai (7) licha ya awali kusitasita kutoa maamuzi kabla ya kujua ratiba ya Pre Season.

Mabosi wa klabu hizo mbili wana urafiki na msimu huu Rais wa Yanga sc Eng.Hersi Said alikwenda nchini humo kuonana na mabosi wa timu hiyo katika kudumisha urafiki wao na hapo ndipo mazungumzo ya mchezo huo yalipoanza rasmi.

Katika maandalizi ya msimu mpya wa 2024/25 klabu ya Yanga itaweka kambi nje ya nchi tofauti na tulivyowazoea kwa misimu iliyopita ambapo wamekuwa wakibaki katika kambi yao ya kila siku ya Avic Town jijini Dar es salaam.

banner

Mastaa wa klabu hiyo ambao hivi sasa wapo katika mapumziko wanatarajiwa kurejea kambini mwanzoni mwa mwezi Julai maalumu kabisa kwa maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu na michuano ya kimataifa huku mpaka sasa kukiwa hakuna uhakika kama timu hiyo itashiriki michuano ya kombe la Kagame Cup inayotarajiwa kuanza Julai 6 visiwani Zanzibar.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.