Connect with us

Soka

Xavi Akubali Yaishe Barcelona

Kocha wa timu ya Barcelona Xavi Hernandez amekubali kuachia ngazi kuifundisha timu hiyo mwishoni mwa msimu huu hasa baada ya kukubali kipigo cha mabao 5-3 kutoka kwa Villareal katika michuano ya ligi kuu nchini humo.

Kocha huyo ambaye alikua staa wa zamani wa kikosi cha Barcelona alipewa nafasi ya kuinoa timu hiyo kukiwa na matarajio makubwa kuwa atafanya vizuri lakini imekua kinyume na matarajio ya wengi baada ya kuwa na mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha klabuni humo.

Kipigo hicho kimeifanya Barca kubaki nyuma kwa alama 10 dhidi ya vinara wa Ligi Real Madrid ambao mapema leo wameendeleza moto kwa ushindi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Las Palmas.

Mara baada ya kipigo hicho cha Barca Xavi ameonekana kuwa na uso wa simanzi nzito akitafakari kabla ya kwenda kutangaza uamuzi huo mgumu ambao ulitarajiwa na wengi.

Msimu huu Barca chini ya Xavi kwenye mechi zake 21 za Ligi imefanikiwa kushinda 13 ikipoteza 3 na kutoa sare 5, ikiwa nafasi ya tatu na alama zao 44 huku Girona wakiwa nafasi ya pili na alama zao 52.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka