Saturday, May 10, 2025
Home Soka Simba sc Waponea Chupuchupu

Simba sc Waponea Chupuchupu

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba sc imeshindwa kuibuka na ushindi dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Simba sc ilianza kupata bao la kwanza mapema kunako dakika ya 11 mfungaji akiwa ni Shiza Kichuya baada ya kipa kuzembea kuokoa mpira uliokua unazagaa langoni bao ambalo lilikuja kusawazishwa na Fulizulu Maganga dakika ya 37 baada ya kuunganisha vizuri mpira wa kona.

Hata hivyo Ruvu Shooting hawana budi kujilaumu baada ya kukosa nafasi nyingi za wazi kufuatia kuimiliki safu ya kiungo baada ya kuwazidi maarifa Mzamiru Yassin na Hassan Dilunga.

banner

Licha ya sare hiyo Simba sc bado wanaendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa ligi kuu kwa kufikisha pointi 72 baada ya kucheza mechi 29.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.